Kamishna Mkuu Msaidizi wa ulinzi na uhifadhi wa UNHCR atoa wito kuongeza kasi katika kupata suluhisho la kudumu kwa wakimbizi nchini Tanzania
Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi na Uhifadhi wa UNHCR, Bi. Ruvendrini Menikdiwela, amehitimisha ziara ya siku tano nchini Tanzania yenye lengo la kuendeleza ushirikiano na serikali, pamoja na ushirikishwaji wa jamii ya wakimbizi katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi waishio nchini Tanzania, hususani wakimbizi kutoka Burundi kwa kuendelea kuwahamashisha kurejea nchini kwao kwa hiari.